Mitandao

WASHITAAKIWA WIZI WA KIMTANDAO WASOTA RUMANDE




Mwanza. Watu watatu wanaokabiliwa na kesi ya wizi wa kimtandao na kujipatia Sh4milioni kwa njia ya udanganyifu, wataendelea kusota rumande hadi Januari 11, mwakani.

Ni baada ya kesi hiyo kuahirishwa kutokana na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Wilbert Chuma anayeisikiliza kuwa likizo.
Washtakiwa hao ni Bony Tefe (40), Mkazi wa Mahina, Spridoni Njunwa (38) wa Igoma na Briton Wilson (43), wa Bugando Mwanza.
Wanadaiwa kusajili namba za simu za uongo na kufungua akaunti Benki ya NMB kwa jina la vyama vya CCM na Chadema wakitaka kuchangiwa fedha za kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25, mwaka huu.
Akiwasomea mashtaka yao jana mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Nyamagana, Gwayo Sumaye, Wakili wa Serikali, Castuce Ndamugoba alidai wanakabiliwa na makosa ya kughushi, kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na wizi kwa njia ya mtandao.
Ndamugoba alidai kati ya Oktoba na Novemba, mwaka huu, washtakiwa hao walikula njama na kutenda kosa la kughushi.
Alidai Oktoba 2, mwaka huu washtakiwa hao walifanya udanganyifu kwa kufungua akaunti Benki ya NMB iliyoonyesha imefunguliwa na CCM Spridon Dini, huku wakijua siyo kweli.
Katika kosa shtaka jingine, washtakiwa hao wanadaiwa kughushi barua iliyoonyesha ilitolewa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na la nne ni kujipatia Sh4 milioni kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Omega wakidai kuwa wao ni wana CCM awasaidie kwa ajili ya kampeni kisha watamfikiria baada ya uchaguzi.
Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote na kurudishwa rumande hadi mwakani kesi hiyo itakapoendelea.

Related

Tech Tips 6811857407621032164

Post a Comment

emo-but-icon

BSC I SEM II DRAFT II TIMETABLE


Ruaha Catholic University

RUCO MIRROR 2014 EDITION

Almanac 2015/2016

Our Facebook Page

.

Portal Admin


ADVERTISEMENTS

soccer league tables

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Our Recent Visitors

item