ZITTO KABWE NA BARUA YAKE YA KUJIUZULU YAZUA MENGINE
 
https://rucuso.blogspot.com/2016/03/zitto-kabwe-na-barua-yake-ya-kujiuzulu.html
Gazeti la  Mtanzania leo March 22 limeripoti kuhusu kamati za Bunge kutarajiwa  kufanyiwa mabadiliko makubwa baada ya ripoti ya uchunguzi wa mwenendo wa  wabunge kuwatuhumu baadhi yao kujihusisha na vitendo vya rushwa kutua  mezani kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Mbunge wa  Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Huduma na  Maendeleo ya Jamii ameandika kupitia mtandao wa kijamii wa facebook  kuwa….
>>>’Kuna  tuhuma za rushwa dhidi ya Kamati mbalimbali za Bunge ikiwemo kamati  ninayohudumu. Nimemwandikia Spika Kuomba Uchunguzi juu Ya tuhuma hizo na  kwamba achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na  vitendo vya rushwa. Nimejiuzulu Ujumbe wa Kamati ili Kutoa Nafasi Ya  Uchunguzi Husika‘
Zitto pia amezungumza na Kito cha ITV na kufafanua zaidi maamuzi yake hayo ambapo amesema..
>>>’ni  vizuri spika aagize uchunguzi wa vyombo vya dola, vyombo vya dola  vikishachunguza ndio hatua ziweze kuchukuliwa kwa sababu kuhamisha tu  watu kwenye kamati haisadii kuweka misingi ya utawala bora’:-Zitto Kabwe
>>>’tuhuma  hizi ni nzito na imekuwa ni kawaida hasa kwa wabunge kutuhumia na mambo  yamekuwa yakiishia juu juu bila hatua kuchukuliwa na hiyo imekuwa  ikishusha hadhi ya bunge kwa hiyo ni vizuri kuhakikisha kwamba jambo ili  linafanyiwa uchunguzi wa kina, ningetaka wabunge wakubali ili  tuchunguzwe ili vyombo vya dola viweze kudhibitisha tuhuma hizi na hatua  sitahiki ziweze kuchukuliwa kwa watu watakaokutwa na makosa’:–Zitto Kabwe




