TUICO YAENDESHA MAFUNZO KWA VIJANA KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI 2019
https://rucuso.blogspot.com/2019/06/tuico-yaendesha-mafunzo-kwa-vijana.html
Wafanyakazi Vijana kutoka katika Taasisi Mbalimbali wakiwa katika Semina ya Chimbuko la Vyama, Jijini Mbeya |
Chama Cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha Huduma na Ushauri kwa kushirikiana na taasisi ya Public Server International (PSI), kimeendesha semina ya sheria za kazi na Chimbuko la vyama vya wafanyakazi kwa wafanyakazi vijana kutoka katika taasisi na makampuni mbali mbali jijini mbeya.
Semina hiyo iliyohusisha pamoja na mambo mengine, kuwajenga wafanyakazi vijana uwezo wa kuzitambua haki zao kazini pamoja na chimbuko la vyama vya wafanyakazi duniani iliendehswa katika chuo cha wafanyakazi Mbeya maarufu kama 'Chuo cha TUCTA' kilichopo Mwanjelwa Jijini Mbeya.
Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Anthony Mavunde katika picha na washiriki |
Mwakilishi wa vijana katika mafunzo hayo Bi. Pendo Simbeye (27) ambaye ni mfanyakazi katika sekta ya Viwanda kutoka katika kampuni ya TBL tawi la Mbeya, alikishukuru Chama Cha Wafanyakazi TUICO kwa kuwapa semina hiyo na kukiri kuwa wafanyakazi wengi vijana hawana elimu ya kutosha juu ya haki za msingi za wafanyakazi.
Kwa
Upande wake, Mwezeshaji katika Semina hiyo kutoka TUICO makao Makuu,
Ndugu Sikunzi John, alisema mafunzo haya yamekuwa yakitolea kila mara
kwa wafanyakazi wa kada mbali mbali na makundi tofauti tofauti.
Aliongeza kuwa lengo hasa la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo
wafanyakazi wa kujiamini na kufanya kazi kwa misingi ya sheria na
utawala bora.
Mwezeshaji wa Semina ya Chimbuko la Vyama, Ndugu Shikunzi John akielezea jambo wakati wa Semina |
Aidha, mkuu wa chuo hicho cha wafanyakazi chenye maskani yake jijini mbeya, Ndugu Edwin Richard Mwakyembe, alikipongeza Chama Cha TUICO na kusema kuwa kwa mtizamo wake TUICO ndio chama cha wafanyakazi pekee nchini Tanzania kinachotekeleza majukumu yake kwa wanachama wake kwa kuwa na watendaji wenye weledi na wabunifu. Aliwahasa wafanyakazi walioko katika sekta zinazohudumiwa na chama cha TUICO kujiunga haraka kwani UMOJA ni Nguvu.
Na: Sebastian Gentanyi
TUICO Makao Makuu
TUICO Makao Makuu