Mitandao

Nyota wa Simba walia ukata

 


By Mwananchi
Dar es Salaam. Baada ya mazoezi ya wiki nzima visiwani Zanzibar kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Azam Jumamosi, kikosi cha Simba kinakabiliwa na mambo mengi yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili timu ifanikiwe.
Kwanza, mishahara ya wachezaji na uwajibikaji wao uwanjani kwani hayo ni mambo yayoweza kuiathiri.
Baadhi ya wachezaji kwenye kikosi hicho kilichojichimbia Zanzibar wamekuwa wakilalamikia kukosa mishahara, huku kiungo Mzimbabwe Justice Majabvi, akisotea nyumba ya kuishi.
Mzimbabwe huyo amekuwa akipigwa danadana na uongozi wa Simba huku akiwekwa Hoteli ya Rombo iliyopo Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam.
Habari za uhakika ambazo gazeti hili lilizipata zinasema kuwa, mchezaji huyo amekuwa akiwasiliana na uongozi wa klabu hiyo mara kwa mara akitaka ahamishwe hotelini hapo ambako wachezaji wote wa kimataifa wa Simba wamefikia na wanaishi wawili wawili chumba kimoja, kitendo chenye kuonyesha kuwakera.
“Tunawaomba wanachama kama inawezekana watuchangie mishahara kama walivyofanya tukijiandaa na mechi ya Yanga, tumechoshwa kulipwa mishahara tarehe 47 na sisi tunazo familia zetu,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba.
“Hebu fikiria, Majabvi alikuwa kwao (Zimbabwe), wamemwita wakamwambia nyumba ipo tayari, matokeo yake hadi leo amewekwa hoteli ya Rombo, hii siyo sawa, wakati mwingine mishahara yenyewe inatolewa kwa mafungu,” alisema mchezaji mmoja wa Simba kwa sharti la kutotajwa jina.
Mchezo huo wa Simba dhidi ya Azam hapo kesho unatarajiwa kuwa mgumu kwa Simba huku Azam ikionekana kujiimarisha zaidi, ingawa Wekundu hao wa Msimbazi wameimarisha kikosi chao kwenye usajili wa dirisha dogo.
Simba imewaongeza kiungo mshambuliaji wa pembeni kutoka Uganda na ambaye alikuwa akiichezea Azam, Brian Majwega, beki Novatus Lufungo kutoka African Sports ya Tanga na Haji Ugando aliyekuwa akicheza soka Italia.
Pia, klabu hiyo imemrejesha kiungo mshambuliaji, Mkenya Paul Kiongera aliyekuwa kwa mkopo katika timu ya KCB ya nchini Kenya.
Mbali ya hao, kupatikana kwa hati ya uhamisho wa kimataifa ya mshambuliaji Daniel Lyanga aliyekuwa akiichezea FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kupona kwa beki mahiri wa kati, Mohammed Fakhi aliyesajiliwa kwenye dirisha kubwa kutoka JKT Ruvu ni faraja kwa Simba.
Uongozi wajibu
Akizungumzia suala hilo la ukata, katibu mkuu wa Simba, Enock Kiguha alisema,“Mishahara tunashugulikia na muda wowote kuanzia sasa tutawalipa, kuna mambo yaliingiliana, ndiyo sababu ya kuchelewa kwa mishahara.
Kuhusu nyumba, Kiguha alisema, “Tayari zimepatikana mbili, moja Sinza na nyingine llala Boma, ile ya Boma atakaa Majabvi na ile ya Sinza watakaa wachezaji wote wa kimataifa.”
Kwa kawaida, klabu hiyo na watani zao, Yanga wana mkataba na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambao pamoja na mambo mengine, unasaidia katika kulipa mishahara ya wachezaji.
Hata hivyo, Simba imepiga bao la kisigino kwenye kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili baada ya kuua ndege wawili kwa mpigo na kuwaacha midomo wazi wapinzani wake kwani imewaongeza kikosini nyota wanne wa nguvu ambao inaamini wataongeza nguvu kwenye kikosi chao kutokana na kiwango na uwezo wao wa uwanjani.
Wachezaji hao ni Novatus Lufunga kutoka Mgambo, Brian Majwega (Azam), Rafael Kiongera aliyekuwa kwa mkopo kwenye timu ya KCB na chipukizi, Haji Ugando aliyekuwa akicheza soka Italia.

Related

Sports 6030760419441150552

Post a Comment

emo-but-icon

BSC I SEM II DRAFT II TIMETABLE


Ruaha Catholic University

RUCO MIRROR 2014 EDITION

Almanac 2015/2016

Our Facebook Page

.

Portal Admin


ADVERTISEMENTS

soccer league tables

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Our Recent Visitors

item