TORRES AIKUBALI TAJI YA MIBA KWA TIMU YAKE
https://rucuso.blogspot.com/2016/04/torres-aikubali-taji-ya-miba-kwa-timu.html

Na Albogast Benjamin
Fernando Torres alianza maisha ya soka katika jiji la Madrid akiwa na klabu yake ya Atletico De Madrid lakini dunia ilimtambua zaidi ndani ya miaka minne aliyokaa Liverpool kuanzia mwaka 2007 hadi 2011.
Baada ya kuhamia Chelsea mambo hayakuwa mazuri kwake na ilipelekea kuuzwa Inter-Milan kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenye klabu yake ya utotoni ambayo haswa ndio masikani yake Atletico De Madrid.
Nyumbani ni nyumabni tu kama ambavyo Gadner G Habash maarufu Captain alivyopokelewa kwa shangwe alivyorejea Clouds Fm ndivyo ilikuwa kwa Torres alivyo pokelewa vyema nyumbani na hapo ndo ilikuwa mwanzo wake kuanza kufanya vizuri tena japo kuwa umri umekwenda.
Kwenye mchezo wa jana wa Uefa hatua ya robo fainali dhidi ya Barcelona alifunga bao la kuongoza dakika ya 25 lakini ilimchukua dakika kumi baadae akapata kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu kiungo wa Barcelona Sergio Busquet dakika ya 36 hivyo kuifanya timu yake ifungwe bao 2 – 1.
Kupitia ukurasa wa twitter Torres amesema haya kuhusiana na kadi hiyo. “I take responsibility for our defeat, but now more than ever let’s go to The Calderón for a comeback #ForzaAtleti”