Katika ukurasa wake wa facebook Mh. Zitto kabwe ametoa mchanganuo huo wenye vyanzo vya upatikanaji wa fedha hizo, huku akisema kiasi kamili cha bajeti hiyo ni kizuri na chenye kuleta matumaini.
“Bajeti ya mwaka 2016/17 ni tshs 29.5 trillions,TRA watakusanya tshs 17.8 trilioni, mikopo itachukuliwa tshs 7.5 trilioni na misaada ya wafadhili 3.6 trilioni, matumizi ya kawaida tshs 17 trilioni na Matumizi ya Maendeleo 11.8 trilioni. Bajeti ya tshs 29.5 trilioni ni hatua kubwa sana”, aliandika Mh. Zitto Kabwe.
Pia Mh. Zitto ameweka wazi kuwa serikali ina mpango wa kukopa kiasi cha shilingi trilioni 2.1, kutoka nje ya nchi, mkopo ambao utakuwa na masharti ya kibiashara.