MAJALIWA: TIMU YA WATU 10, DODOMA MPYA
 
https://rucuso.blogspot.com/2016/10/majaliwa-timu-ya-watu-10-dodoma-mpya.html
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema  Serikali imeunda timu ya wataalamu ambao watatoa ushauri juu ya suala  zima la kuhamishia makao makuu Dodoma.
Ametoa kauli hiyo  wakati akizungumza  na watumishi wa Serikali wa mkoa wa Dodoma, wazee wa mkoa huo,  wafanyabiashara pamoja na viongozi mbalimbali kwenye ukumbi wa mikutano  wa Dodoma (Dodoma Convention Centre). Bila  kutaja majina ya wajumbe wa timu hiyo, Waziri Mkuu amesema timu hiyo  itaongezewa wataalamu kutoka China na Malaysia ambao nchi zao tayari  zina uzoefu wa kuhamisha makao makuu ya nchi zao zaidi ya mara moja.
Bila  kutaja majina ya wajumbe wa timu hiyo, Waziri Mkuu amesema timu hiyo  itaongezewa wataalamu kutoka China na Malaysia ambao nchi zao tayari  zina uzoefu wa kuhamisha makao makuu ya nchi zao zaidi ya mara moja.
“Tumeunda timu ya watu 10 ambao ni  wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa miji mikuu, hawa wana  uzoefu wa kuangalia makao Makuu ya nchi yanafananaje. Watakuja Dodoma,  wapitie master plan na kisha watapita kwenye maeneo kadhaa ya mji ili waone hali halisi ikoje ndipo watupe maoni yao,” amesema.
“Tunataka tusirudie kosa la Jiji la Dar  es Salaam la kulazimika kubomoa makazi ya watu kila inapolazimu kufanya  uboreshaji wa miundombinu. Hawa watu watatuambia wapi tunatakiwa tuweke  njia nne au sita za magari, wapi tuweke bustani au wapi tujenge nyumba  za ghorofa moja, mbili, tatu au zaidi,” ameongeza.
Akifafanua kuhusu miundombinu, Waziri  Mkuu amesema timu hiyo pia itatakiwa kutoa ushauri juu ya wapi ijengwe  njia ya malori tu au mahali gani zinahitajika kujengwa barabara za juu  (flyovers) ili kuepusha msongamano katikati ya mji wa Dodoma.