BAADHI YA OMBAOMBA NI MAWAKALA WA DAWA ZA KULEVYA
 
https://rucuso.blogspot.com/2016/04/baadhi-ya-ombaomba-ni-mawakala-wa-dawa.html
MKUU wa Mkoa Dar es Salaam, Paul  Makonda amesema kwa mujibu wa utafiti alioufanya, ombaomba walioko  jijini Dar es Salaam baadhi yao wanajihusisha na uuzaji wa dawa za  kulevya.
Akihojiwa katika mahojiano ya moja kwa  moja na kituo kimoja cha redio, Makonda alisema wapo watu ambao  wanatumia mwanya huo kusambaza dawa za kulevya. “Wapo  wanaotumia fursa hii kusambaza dawa za kulevya kwa sababu anavyopita  huwezi kumhisi kwa namna anavyoonekana, lakini watu hawa ni miongoni mwa  mawakala wa kusambaza dawa za kulevya,” alisema Makonda.
“Wapo  wanaotumia fursa hii kusambaza dawa za kulevya kwa sababu anavyopita  huwezi kumhisi kwa namna anavyoonekana, lakini watu hawa ni miongoni mwa  mawakala wa kusambaza dawa za kulevya,” alisema Makonda.
Makonda aliwataka wakazi wa jiji hilo  kushirikiana naye katika kuwaondoa ombaomba hao ambao wengi wanatoka nje  ya Da es Salaam na kwamba hakuna tija kuendelea kuwaacha. “Watanzania  tuna upendo sana lakini tunahitaji kutafakari kama kweli watu walioko  barabarani wakiomba kama kweli wanahitaji msaada huo au la,” alisema  Makonda.
Alisema kwa kuendelea kuwaacha ombaomba  hao pia kutasababisha vijana ambao sasa wanaomba barabarani kuwa watu  hatari katika maisha yao ya baadaye kwani wakikosa pesa wataingia katika  shughuli za uporaji ili wapate fedha.
“Itafika kipindi ataanza kuangalia kile  alichokuwa anakikusanya wakati akiomba na kile anachokipata akifanya  kazi, ataona akifanya kazi hapati kiasi kikubwa, ataamua kuwa mporaji,”  alisema Makonda.
Makonda alisema kwa mujibu wa utafiti  alioufanya, asilimia 80 ya ombaomba wanatoka nje ya Dar es Salaam na  kesho operesheni ya kuwaondoa watu hao itaanza rasmi huku wale ambao  hawana ulemavu wowote wakikamatwa kwa makosa ya uzururaji.