Aprili 7, 2016: Ambayo ni siku ya pili ya ziara yake nchini Rwanda, Rais Magufuli atajiunga na wananchi wa Rwanda katika kumbukumbu ya miaka 22 ya mauaji ya kimbari nchini humo ambapo watu takkribani milioni moja walipoteza maisha, wengi wao wakiwa Watutsi.
Baadaye Aprili 7, marais hao watajiunga na wananchi katika “Walk to Remember” kabla ya kuhudhuria mkesha wa kumbukumbu hizo katika uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Rwanda. Rais Magufuli pia ataweka shada la maua katika mnara za kumbukumbu za mauaji hayo.